Hapajulikani atakapozikwa Robert Mugabe. Familia yafanya uamuzi tofauti

p07n1lng
p07n1lng
Ni kweli kwamba anapoaga mtu,watu wa familia huwa na usemi mkubwa kuhusu jinsi watakavyofanya desturi za mazishi.

Taarifa zipo kwamba familia ya marehemu Robert Mugabe na serikali ya Taifa la Zimbabwe inayoongozwa na Emmerson Mnangangwa wanahitilafiana kuhusu atakapozikwa Robert.

Mwili wa mwendazake Robert Mugabe ulitua uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege wa Robert Gabriel Mugabe uliopo jijini Harare jana jumatano.

Muasisi huyu wa taifa tukufu la Zimbabwe atapumzishwa pahala pasipojulikana.

Soma hadithi nyingine:

Hii ni kufuatia hali ya kutoelewana miongoni mwa wanafamilia na serikali.

Mugabe ni kati ya mibabe ya viongozi wa Afrika.

Mwanasiasa huyu aliitawala taifa hili lililopo kusini mwa Afrika kwa muda wa miaka 37.

Alikuwa dikteta na uongozi wa kiimla ulikuwa falsafa na nguzo kuu ya kuiendesha Zimbabwe.

Mwezi wa Novemba mwaka wa 2017 jeshi lake mwenyewe lilimbandua uongozini.

Soma hadithi nyingine:

Hali ya ugonjwa ilimzidia na baada akafariki hospitali ya GlenEagles nchini Singapore.

Vita vya kuvutana ni wapi atazikwa vinamfedhehesha sana rais Emmerson Mnangagwa na zaidi ya hapo kusababisha nyufa katika chama tawala cha ZANU-PF.

Mugabe anatakiwa kuzikwa siku ya jumapili.

Soma hadithi nyingine:

Chama cha rais Mnangagwa kinapendekeza Mugabe azikwe katika eneo la mnara uliozikwa mashujaa waliopigania taifa hilo katika vita vya ukombozi.

Kwa upande mwingine wanafamilia na watu wa ukoo wa Mugabe wanakataa katakata mpango huo na kutaka azikwe kijijini.

Uamuzi wa wanafamilia umejikita katika misingi ya uchungu kwamba rais Emmerson alitumia njia za mkato na kuipindua serikali yake.

Mazishi yaliyoratibiwa jumapili ijayo Tarehe 15 yatategemea majadiliano ya pande mbili zinazohusika. Familia na serikali.