harmonize_smoking1__1569070400_60600

Harmonize ataja mastaa Tanzania waliojunga na Konde Gang, aitaja WCB

Staa na nyota wa Bongo Harmonize ametaja baadhi ya majina ya watu ambao watakuwa katika lebo ya Konde Gang.

Ikumbukwe kuwa staa huyu ndiye kifungua mimba cha lebo kubwa Afrika Mashariki ya WCB iliyopo mjini Dar nchi jirani ya Tanzania.

Harmonize almaarufu kama Konde Boy amekuwa mkubwa kwa kupiga nyimbo hatari na kushirikisha mastaa wakubwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Nigeria kati ya nyinginezo.

Matamasha anayoyafanya ni makubwa sawa na bosi wake Diamond Platnumz.

Soma hadithi nyingine;

(+Meseji zavuja ) Willy Paul aonywa, meseji za ufisi Insta

Dogo ana mpenzi wa haiba ya juu sana Sarah.

Ana walinzi sawa na idadi ya Diamond. Kumewahi kutokea vyombo vya habari nchini Tanzania zinazowalinganisha wawili hawa.

Katika mahojiano, staa huyu aliitetea Konde Gang na kutaja watu walio katika lebo hiyo,

“Sisi tunakuwa kila siku na watu wanatupenda. Jamii inatupenda na inatufuatilia sana. Konde Gang ni still WCB.”

“Konde Gang itakuwa na mastaa wa wengine sio mastaa. Nadhani kwa sasa umeona Jose wa Mipango Jabulanti, Choppa,Mnyama Mkali, Budda na Mchachambo .”

“You know Young Money right, you know cash money right. Come on why are you asking?” Alisema Harmonize.

Kwa usemi huu, staa huyu anasema hana matatizo na WCB.

Soma hadithi nyingine;

Zitakavyofanyiwa noti mzee za elfu, M-Pesa kukoma kuchukua Alhamisi

 Hii inatokea kuwa tofauti na matendo yake baada ya kufanya hafla ya ndoa na kukosa kuwaalika mastaa wa WCB

Wanandoa hawa walihakikisha wameipanga hafla hiyo kwa mbwembwe zote na hawakuwaalika mastaa wa WCB.

Soma hadithi nyingine;

Mkali wa “Lubbish” apigwa faini ya 1M kwa kuonyesha video chafu, ajitetea

Mzee Abdul anahoji kuwa dalili za Harmonize kuwa ana uwezo wa kufanya na kusimamia fiesta zake nje ya nchi ni ishara kuwa mwana kashakua na kwa hivo kutoka kwake ni kwema kwa maslahi yake.

Anadokeza kuwa labda dogo kapewa ushawishi na marafiki wake ili kufanya uamuzi huo.

”Kwanza Naseeb alimuangaikia sana. Kamtufuta kampa sapoti kubwa kamtoa kimuziki,” Mzee Abdul.

“Harmonize sio mtoto. Ukiona mtu anatoka kashakomaa tayari.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments