Harmonize kuitema WCB ni njama ya Mondi kusahaulisha Kiba kwenye tasnia

HARMONIZE
HARMONIZE
Idadi kubwa ya mashabiki wa Bongo Fleva mpaka sasa hawaamini kuwa ni kweli staa wa bongo Harmonize kwa kweli ameitema lebo iliyomkuza. Hawaamini ni kosa gani msanii huyu alikosewa ili aamue kufanya uamuzi wa ghafla na wenye uzito kama huo.

Hakuna siku mpaka sasa Harmonize ametokea kusema masaibu yaliyomkuta ili kutoka katika lebo kubwa Afrika Mashariki. Wengi wanahoji kuwa ni njama ya Diamond Platnumz kumfanya Harmonize awe mkubwa ili kutoa dhana ya mashabiki kila mara kumlinganisha na hasimu wake Ali Kiba.

Som hapa pia:

Kwa sababu kwa sasa Harmonize anachonganishwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni mkali kulika Diamond. Wema Sepetu aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platnumz siku za jadi aliwahi kunukuliwa akisema kuwa dogo Konde Boy yuko sawa kimuziki kushindi Diamond.

Sasa mashindano yanatengenezwa na vyombo vya habari kati ya Harmonize na Diamond. Jambo kama hili huenda likasababisha Ali Kiba kupotea masikioni mwa watu na ata kukosa kuonekana mbishi wa karibu wa nyota na staa anayemiliki lebo ya Wasafi.

Som hapa pia:

Je, unaamini hii inaweza kuwa sababu ya Harmonize kuitemana na WCB na mazingira yatengenezwe ya chuki kumtoa Kiba kwenye tasnia ya muziki. Tupe maoni.