'Hata kwa kifo upendo wa mama hauishi,' Mama wa Rev Peter Kania amuomboleza

116433637_2731199850537720_4046527630804440808_n
116433637_2731199850537720_4046527630804440808_n
Kwake Damaris Nyandia Kariuki kifo cha mwanawe Reverend Peter Kanai hakijaweza zusha imanai yake kwa Mungu, alisema haya alipokuwa anamuomboleza mwanawe.

Peter kabla ya kifo chake alikuwa katibu mkuu wa kanisa la Presbyterian Churches of East Africa (P.C.E.A), na kuaga  kwa ajili ya virusi vya corona.

Akizungumza wakati wa hafla ya mazishi hayo alisema kuwa alikuwa amempeana mwanawe kwa Mungu na alitenda alichokuwa amepanga Mungu.

"Kania mwanangu nakumbuka vile ulikuwa mchanga na vile umekua kwa immani, nilikulea na kukupeana kwa Mungu ili umtumikie, sina hisia mbaya kwa maana umefariki

Ulinipenda na ukanisadia kwa vyovyote vile nilivyokuwa nahitaji, ulihakikisha nimeishi maisha mema, marafiki wako wote wamekuwa wanangu kwa maana uliwatambulisha kwangu

Familia yako ulioacha nyuma, Mama Njeri,Njeri,Kariuki na Joel sasa ni wanangu Moyo wangu umepumzika kwa kujua uko na mwenyezi Mungu." Alizungumza.

Pia alimshukuru kwa kumuachia watumishi wa Mungu, amabo watamlinda wakati hayupo tena,

"Nina shukrani nyingi kwa kuniachia watumishi wa Mngu kama Reverend Caro watakao nilinda kama huyuko, najua siyuko pekeyangu siana maneno yakutosha ya kunakili kueleza jinsi nimehuzunika siku hii ya leo

Upendo wa amamkwa mwanawe huna mwisho, huwa unakua na unakua na unazidi kukua hata baada ya kifo, mwanangu umepigana vita vyema

Umemaliza mbio zako umekaa na imani(2 Timotheo4:7) lala salama mwanangu, tutapatana tena mbinguni kwa maana hapo ndipo tunaelekea."