Hatari! Watu 12 waliokuwa wamewekwa kwenye karantini katika mpaka wa Tanzania na kaunti ya Migori wametoroka

unnamed (28)
unnamed (28)
Mazingira duni na miundo msingi mbovu katika kituo cha kuweka watu kwenye karantini katika shule ya upili ya Mabera kaunti ya Migori inasemekana ndiyo ilichangia pakubwa kutoroka kwa jamaa 12 waliokuwa wamezuiwa kwenye kituo hicho.

Kituo hicho kinapatikana enebunge la Kuria Magharibi ambayo inapakana na taifa jirani la Tanzania,Kulingana na taarifa ,jamaa hao wanaripotiwa kuhepa kwenye kituo hicho mida ya saa 12 usiku .

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Isebania ,walidhibitisha tukio hilo saa nane baada ye baada ya jamaa hao kutoroka na kunakili tukio hilo katika kitabu cha OB nambari  30/22/5/2020.Watu wengine 20 wamewekwa  kwenye karantini.

David Marwa Ikarai ,mhudumu  wa afya ambaye aliandikisha taarifa hiyo amesema kati ya watu 20 waliozuiliwa kwenye kituo hicho ,Erick  Otieno na Wyclife Opombe ndio tu walipeana taarifa za Ukweli na wengine wakakataa.

“Twelve of them with their unknown identities had escaped to unknown destination. Scene visited by police and search is underway,” Taarifa hiyo ilisema.

Mkuu wa afya kaunti ya Migoro Isca Oluoch na afiusa mkuu wa Polisi Mabera Cleti Kimayo wamedhibitisha tukio hilo.

Wamesema hatua ya kuwatafuta watu 12 waliotoroka imeanzishwa mara moja .

Yanajiri hayo huku serikali ikianza kuhofia kutokana na hatua ya baadhi ya wakenya kuanza kutoa taarifa za uongoz wanapojiwasilisha katika vituo vya kupimwa .