Hatimaye Anerlisa Muigai Apatana na Mtoto wa Ben Pol (Picha)

Latifah Mohammed
Latifah Mohammed
Ben Pol, mwanamziki maarufu wa nyimbo za bongo, ana mtoto wa miaka tano. Pol amezaa na Latifah Mohammed, aliyekuwa malkia wa urembo Tanzania mwaka wa elfu mbili kumi na tatu.

Wawili hawa hawako pamoja sasa lakini wanashirikiana vizuri kutimiza majukumu yao ya uzazi.

Anerlisa Muigai amethibitisha kuwa tayari amepatana na mtoto wa Ben Pol na kupitisha wakati pamoja.

Katika mahojiano ya awali, Latifah alifichua jinsi ilivyokuwa kuonana kimapenzi na mwimbaji huyo wa Tanzania;

''Unajua nimepatana na watu wengi tofauti. Mtu anaweza ingia katika maisha yako na mategemeo kadhaa na mwishowe awe hajaridhika hivyo aende. Kwa hivyo ukimpata mtu ambaye anakuelewa, inahimiza sana.''

Katika mahojiano mengine na Mo Fave, Latifa aliweka wazi kuwa yeye huwa mtulivu ata baada ya kuona Ben Pol akizungumza na kuwashirikisha mashabiki wake wa kike.

''Sioni tofauti yoyote kati ya kumuona kimapenzi na kumuona mtu wa kawaida. Huwa hafanyi matendo yake kama mtu mashuhuri. Unafaa kumuelewa vizuri sana. Hufai kupandwa na mori wala kutenda mambo ya kijinga wakati unamuona anahusiana na mashabiki wake wa kike akitumbuiza kwenye jukwaa na wakati hayuko kwa jukwaa. Unafaa kuwa mtulivu na usiwe mwepesi wa kuhukumu jambo lolote.''

Anerlisa Muigai na mchumba wake wamekuwa hawashikiki tangu wachumbiane mwishoni mwezi jana. Pol alienda chini kwa goti lake na kumposa Anerlisa huku akimtunukia sifa nyingi sana.

Anerlisa alikiri kuwa Mungu alikuwa amembariki na vitu vingi sana ila hangeweza kulinganisha na kuwa na mtu anayemfanya apende tena na tena, mtu anayemfanya awe mpole na juu ya yote mtu anayemfanya awe mcha Mungu na kuwa angemchagua yeye tu wakati wowote.

Kumekuwa na madai kuwa wawili hawa waweza kuwa wanatarajia mtoto huku Bi Muigai akichochea zaidi kuwa alitaka pacha ambao wanafanana Ben Pol.

Wawili hawa wamekuwa katika mahusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Anerlisa aligusia kuwa wanatarajia kufanya harusi kubwa sana.

Swali sasa ni? Wawili hawa watafunga ndoa lini? Je kati ya ndoa yao na wachumba wa Tanzania na Kenya, Diamond na Tanasha ni gani itavuma zaidi?

Ni wakati tu utathibitisha.