Hatua za mwisho! Mutahi ,Matiang'i na Magoha viongozi wa dini

EZvDlbZXQAg6lUJ.jfif
EZvDlbZXQAg6lUJ.jfif
Wakenya wakiwa wanasubiri kwa hamu na ghamu kuhusiana na hotuba ya rais Kenyatta hapo kesho kuhusu iwapo kiongozi wa taifa atakuwa anaondoa baadhi ya masharti yaliyowekwa nchini. Mawaziri watatu, Mutahi Kagwe wa afya, George magoha wa Elimu na Fred Matiang'i wa usalama hii leo wamefanya kikao na washikadau kutoka dini mbalimbali ili kubaini namna ya kufunguliwa kwa makanisa nchini.

Kando na kukutana na viongozi wa dini, mawaziri hao pia wamekutana na washikdau katika sekta ya Elimu ili kubaini baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuhusiana na kufungwa kwa shughuli ya masomo nchini kutokana na corona.

Rais Uhuru Kenyatta anatazamia kuzungumzia taifa hapo kesho baada ya masharti yaliyokuwa yamewekwa na serikali kufikia kikomo.

Aidha wakizungumza na wanahabari baada ya mkutano huo, viongozi wa dini nchini wamesema wanaunga mkono masharti yaliyowekwa ili kuzuia maambukizi zaidi.

Kwa upande wake Matiang'i, amewashukuru viongozi wa dini kutokana na uvumilivu waliochukuwa.

Amesema maafikia yao hii leo yatafikishwa kwa kiongozi wa taifa na wakenya kufahamishwa hapo kesho wakati ambapo rais atakuwa analihutubia taifa.