wambui bob collymore

‘Hatuna wakati wa kuharibu,’ Wambui Collymore azungumza baada ya haya kufanyika

Mjane wa aliyekuwa mkurugenzi muu wa kampuni ya Safaricom Bob Collymore, Wambui Collymore amesuta vikali wanahabari baada ya wasia wa mwendazake kufichuliwa.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter Wambui alisema kuwa kwa mara amezima wanahabari kutokana na mambo kadha wa kadha na kusema kuwa maisha yake si habari muhimu.

Bob-Collymore34

“Tangu mwaka wa 2016 wakati jina langu na maisha yangu yalikuwa kwenye vyombo vya habari nimefanya mahojiano mengi na hata kuzima mengi kuliko vyenye nilikuwa nimekubali

Mengi ya mahojiano yanahusu kazi ambayo nafanya na yamewatia wengi nguvu, hoja yangu imekuwa kuwa maisha yangu hayawezi kuwa habari.” Alizungumza Wambui.

https://twitter.com/WambuiKamiru/status/1305830531553284096

Wambui alizidi na kusuta wanahabari huku akisema kazi yao ni kujulisha,kuelimisha na hata kuwapa watu nguvu na wala si kuharibu wakati wa hadhira.

“Wakenya wana uwezo wa mabadiliko makubwa, wakenya wana uwezo wa uvumbuzi na uwezekano mkubwa,vyombo vya habari havipaswi kuharibu wakati wa kutufanya tuamini hamna habari kamwe

Pia hatuna wakati mwingi wa kuharibu, mimi si habari, habari ni kuhsu vile tunaishi kwa giza, vyombo vya habari vinaweza amua maisha yetu ya usoni ya nchi yetu kila siku.” Aliandika Wambui

 

Photo Credits: maktaba

Read More:

Comments

comments