Heka Heka! Mwanamke amshika kamanda wa polisi kimaso kwa kukosa kujukumikia majukumu yake

gruCfJjL.jfif
gruCfJjL.jfif
Kihojacha kushtukiza kimeshuhudiwa hii leo katika kaunti ya Embu mjini baada ya mwanamke mmoja kukabiliana na kamanda wa polis aliyestaafu kwa kukataa kushughulikia wanawe.

Akiwa na mori na hamaki,mwanamke huyo alimshika dhabiti mwanamume huyo kutoka upande mmoja wa barabara hadi upande mwengine akimshinikiza kujumikia majukumu yake kama mzazi.

Katika video hiyo inayosambaa mitandaoni ,mwanamke huyo anasisitiza mume huyo kumpatia shilingi laki mia 300 ili kusaidia wanawe.

Amemkashifu afisa huyo aliyetambulika kama Mureithi na ambaye anasema alikuwa anafanya kazi katika eneo la Voi kabla ya kustaafu na kukataa katakata kuwajibikia swala lake..

"He has refused to take responsibility as the father and he has retired. How does he want me to take care of the kid? Take his photos he was a base commander but has now retired...I need KSh 300, 000 for upkeep as you promised," alihamaki mwanamke.

Jaribio la umma kujaribu kumuokoa afisa huyo liliambulia patubu baada ya mama huyo kuendelea kumrushia cheche za maneno afisa huyo.

Kwa muda kama wa dakika kumi hivi,maafisa wa polis walilazimka kuingilia kati kumuokoa mwenzao aliyestaafu huku mmoja wa afisa aliyekuwa amejihami akionekana aktuliza mambo hayo kwa njia ya utulivu.

"Coronavirus aside. I want my Ksh 300k child upkeep," "I will never go to court neither will you take me to the station. My father is a retired cop too," mwanamke huyo alimaka.