Hello zari? Dry spell inanimaliza, tunaaweza rudiana?-Diamond amwandikia ujumbe Zari baada ya kuachana na Tanasha

NA NICKSON TOSI

Zari Hassan kwa muda sasa amekuwa akimkashifu pakubwa msanii wa Tanzania Diamond kutokana na tabia zake za kuhanyahanya na kutamani kila mwanamke anayemuona mbele yake.

Kwa sasa Zari ameibua kuwa alipokea ujumbe kutoka kwa mpenzi wake wa zamani Diamond akisema kuwa anakosa penzi lake na angependa iwapo kama wangeonana.

Nimepata ujumbe kutoka kwa EX wangu akisema ananikosa sana na angependa tukutane naye, lakini nilimwambia kuwa sina muda na nilikuwa nimeenda kuhudhuria mazishi. Aliniuliza aliyekuwa ameaga. Alisema Zari katika video

Zar alitengana na Diamond mwaka 2017, siku ya kusherehekea Valentino kwa kile alisema ni mtu anayependa mipango ya kando kwa wingi.

 Aliongeza kuwa tangu waachane na Diamond, hajawahi shughulikia mtoto wake