mIGUNA MIGUNA

HELL:Wakili wa Miguna Miguna asema mteja wake anapitia mateso Ulaya

Jitihada za Wakili Miguna Miguna kurejea nchini zimepatwa na  pigo jingine baada ya mahakama kuahirisha kesi yake hadi machi tarehe 23 machi . Wakili wake John Khaminwa  amefichua kwamba mteja wake anaipitia mahangaiko barani ulaya .Khaminwa  alikuwa akijibu hatua ya mahakama kuisongesha kesi yake hadi  Machi bila yeye kuwepo .

Kenya Ina Mambo! Video ya Jamaa mmoja akipiga punyeto hadharani yawashangaza wanamitandao

Ameshtumu wakili kutoka afisi ya mkuu wa sheria kumruhusu hakimu kuisikiza kesi hiyo  saa tatu asubuhi ,saa mbili mapema kuliko muda ambao kesi hiyo ilifaa kusikizwa saa tani asubuhi kabla hajafika  kortini .Khamninwa  amesema atawasilisha kesi kortini kupinga kusongeshwa kwa kesi hiyo hadi tarehe 23 machi  anayosema ni mbali sana . Wakili wa tume ya kitaifa ya kutetea haki haki za binadamu  Victor Kamau alikuwa kortini wakati uamuzi huo ilipotolewa .

DISARMED AND HOPLESS: Wafahamu Viongozi 7 watakaopokonywa ulinzi wa polisi na Bunduki .

Jaji wa mahakama kuu  John Mativo  alikuwa amemwagiza mwanasheria mkuu Kihara Kariuki  kutoa maoni ya ushauri  kueleza mbona aserikali ilikuwa imekiuka agizo la kufanikisha kurejea nchini kwa Miguna . Kihara  alimtuma  mwakilishi kortini  lakini mawakili wa Miguna walimkataa  wakisema suala hilo lilifaa kushughulikiwa na mkuu wa sheria mwenyewe . katika uamuzi wake jaji Mativo  alisema mwanasheria mkuu kama ‘rafiki’ wa mahakama alifaa kutoa maelezo  kuhusu hatua ya serikali kukataa kufanikisha kurejea nchini kwa Miguna .

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments