Hila kwenda kombo!! Mwanamke anaswa akijaribu kuiba mtoto

IMG_20190710_090049_0 (1)
IMG_20190710_090049_0 (1)

Maafisa wa polisi wa kituo cha Webuye wanamzuilia mwanamke mmoja wa miaka 22 kutoka nchi ya Uganda ambaye anashukiwa kupanga njama ya kuiba mtoto katika hospitali ya Kimishen ya Lugulu eneo bunge la Webuye, kaunti ya Bungoma usiku wa kuamkia leo.

Josephine Nafuna, ambaye ameoleka hapa inchini Kenya eneo la Kamukuywa eneo bunge la Kimilili alikuwa amefikishwa katika hospitali hio kujifungua na kumbe hakua mjamzito.

Msimamizi wa hospitali ya Lugulu Jackson Fuko amesema kwamba wauguzi walipomchunguza mama huyo walimpata na viraka tumboni huku akikiri kwamba alikua na mimba hapo awali lakini alipoteza na alikua anaogopa kuachwa na bwanake baada ya mimba zingine nne kutoka katika ndoa zake mbili za hapo awali.

OCPD wa Bungoma mashariki Valerian Obore amesema  kwamba maafisa wa polisi wameanzsiha uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.

Soma megi