Soma hapa hadithi nyingine:
https://www.instagram.com/p/BzDJo8MnP0N/
"Ukisema nifanye kiki nitakuwa sasa mimi sio mwanamuziki. Itakuwa sasa mimi ni Ringtone.Sitakuwa mwanamuziki." HopeKid.
"Maneno ya Ringtone ni magumu sana. Ni rafiki yetu. Ni ndugu yetu mkubwa. Hatumwelewi kabisa pia sisi. Naweza penda sana kufanya muziki na yeye." Alimdokeza mtangazaji Rais Papa.
Tazama hapa:
HopeKid ambaye anafanya muziki wa New School Dancehall sasa anatamba freshi na kibao hatari cha Control Me anazidi kutia fora katika tasnia ya muziki wa injili hapa nchini.
Staa huyu amesimulia Rais Papa jinsi angetamani sana kufanya nyimbo na staa wa muziki Chris Martin. HopeKid kwa sasa ni balozi wa Autism Lights. Autism au tawahudi ni ugonjwa wa ngozi unaomfanya mtu kuonekana ni kama amechomeka.
Mapema mwakani muimbaji huyu alikuwa amechonganishwa katika skendo na mwenzake Dk Kwenye Beat. HopeKid anasema kuwa walisuluhisha swala hilo na kwa sasa wako freshi.
"The whole story was resolved na tuka-move on." amesema HopeKid
"Dk tumegrow na yeye. He's a brother to me."