"Hospitali ilikataa kugeuza sehemu zangu nyeti,"-Audrey

D_irJBMXkAAVGxw__1562151849_82571
D_irJBMXkAAVGxw__1562151849_82571
Audrey Mbugua ameitaka serikali iweze kuwatambua raia waliozaliwa na "jinsia mbili". Katika mahojiano na kituo cha Jambo, Audrey ambaye zamani alifahamika kama Andrew na kuibadilisha jinsia yake amefunguka mwanzo mwisho na kusema kuwa uongozi wa hospitali ulikataa kumbadilisha sehemu nyeti za kiume na kumpachika za kike.

Soma hapa:

"Kitambulisho kinasema mimi ni Andrew Mbugua. ID na passport zinaonyesha mimi ni mwanaume . Nikitoa pesa kwa Mpesa huwa wananiuliza madam mbona ID yako inasema wewe ni mwanaume." alisema Audrey.

Audrey anasema kuwa wazazi wake huwa wanachanganyikiwa na hali yake na kumuita kama mwanamme.

"Sometimes huwa wananiita "He'....babangu na mamangu hawajazoea kuniita "She". Alisema Audrey.

Audrey anasema kuwa ilimbidi akaacha hasira na kukubali hali yake.

"Kuwa na machungu mengi ni mimi nitaumia. Ni mimi nitakuwa na presha."

Soma hapa:

Audrey anaeleza kuwa kuna utaratibu wa kufuata katika kubadilisha jinsia kwenda nyingine. Juhudi za Audrey ziligonga mwamba wakati madaktari walisema wanahitaji wazazi wake ili waweze kuidhinisha upasuaji.

"Sikuweza kupata uwezo wa kubadilisha sehemu zangu nyeti. Viongozi walitaka idhini ya wazazi ili kubadilisha sehemu zangu nyeti. Hauhitaji ruhusa kugeuzwa vitu pale chini." Alihoji Audrey.

Audrey aliwahi kupata ushindi kupitia mahakama kuu ili kupata vyeti vyake vya shule kubadilishwa jinsia na jina lake.