Hospitali zachunguzwa kwa madai ya kutotoa huduma za dharura kwa wagonjwa

Picha kwa hisani ya: mwakilishi.com

Hospitali za kibinafsi na za umma zinachunguzwa kwa madai kwamba zimekataa kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa  wanaokimbizwa katika taasisi hizo.

Gavana wa Nairobi Evans Kidero amesema hospitali zitakazopatikana na hatia, hazitopewa leseni mpya za kuhudumu. Hii ni baada ya mwanamme mmoja kuaga dunia wiki jana baada ya kungoja kwa zaidi ya saa 18 ili kupewa huduma za dharura katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na zingine za kibinafsi.