huddah (1)

Huddah, kabla utoke kwenye mitandao umempa Khaligraph ”kisima cha asali” ulivyodai?

NA NICKSON TOSI

Huddah Monroe amekuwa mitandaoni siku za karibuni na msanii Khaligraph Jones baada ya kudai kuwa iwapo msanii huyo hatawacha hulka ya kumtaja mitandaoni, basi atampa taw twa twa vya kutosha ndiposa amkome. Amedai kuwa anapania kuchukuwa likizo ya muda kutoka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusemwa kila mara na watu.

Uamuzi huu wa Huddah umewaacha wengi waliokuwa wanasubiri kuona majibizano zaidi baina yake na Khaligraph yakiendelea.

Katika ujumbe alioandika kwenye mojawapo ya vitandawazi vya kijamii Huddah alisema hivi.

“Nachukuwa likizo kutoka kwa mitandao ya kijamii kwa muda, taarifa zinazoandikwa kunihusu mimi zinaniathiri kweli kiakili. Mwanzo ilikaa kama mchezo tu, lakini kwa sasa imenifikia kooni, na jinsi ninavyoona taarifa hizo ndivyo zinavyoniathiri mimi. Aliandika Huddah.

Huddah in white

Katika jumbe zingine alizodai kuwa huenda ni za mwisho kuandika kwenye mitandao yake ya kijamii, Huddah aliwarai wananchi kuheshimu wosia wa serikali ili kuepukana na virusi vya Corona ambavyo vimeathiri mataifa mengi duniani.

Tukae nyumbani. Tusalie tukiomba na tutarajie mema mbeleni kutokana na jitihada ambazo serikali imechukuwa kuhakikisha kuwa wanakabiliana na Corona. Aliandika Huddah.

huddah

Kwa sasa kichuna huyu anaishi Dubai na mpenziwe wa sasa baada ya kudai siku za hivi karibuni kuwa alimaliza kuchumbiana na wanaume kutoka Afrika Mashariki.

 

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments