Huduma kubadilisha vitambulisho na nyaraka za kirasmi kwa njia ya kijitali

Seikali ina mpango wa kubadilisha vitambulisho pamoja na nyaraka za kirasmi kuwa katika njia za kijitali, hii ni baada ya kufuatia shambulizi la DusitD2 lililofanyika mwezi jana.

Kuanzia machi, 15, wananchi wanaeza kosa kuwa wakibeba vitambulisho kwa maana serikali itakuwa na maelezo wanayohitaji kutoka kwa mwananchi.

Cheti cha KRA, cheti cha good conduct na kadi ya NHIF na NSSF zinaeza kuwa hazina kazi tena katika mwananchi.

Mradi huu utachukua takriban millioni 6 huku kila mwananchi akipewa nambari itakayomtambulisha katika maeneo mbalimbali.

Pia waziri wa mambo ya ndani amesema kuwa teknolojia hii itawezesha kuwa na utaratibu wa kujitambulisha, na mwananchi ambaye ako na miaka 6 kusajiliwa katika teknologia hii mpya.

Miaka ambayo imepita serikali ilikuwa inapeana kitambulisho kwa mtu tu ambaye amefikisha miaka 18, ambayo ilikuwa itasisitiza sana katika cheti cha kuzaliwa.

"Wananchi wako na hati nyingine za kubeba, ukusanyaji mkubwa wa kadi ya serikali ambayo inahitaji kukusanya na kusajili ujumbe sawa.

"Tulikubaliana kuwa data zitaweka maelezo hayo katika chanzo kimoja,  tu kadi moja ndiyo itakayotumika kutambulisha mtu,"PS Karanja Kibicho alieleza.

Serikali itahitaji picha ya digitali, maelezo kuhusu wazazi, maelezo yaliyoko katika cheti cha kuzaliwa, mahali pa kuzaliwa, kaunti, kata ndogo ya kaunti, hadhi ya kindoa, kiwango cha elimu, hadhi ya kuajiriwa na kabila.

Kusajiliwa huko pia kutahitajika watu kusema kama wako katika kilimo na kiwango cha shamba ambalo wana lima.

Kuanzia hapo mwananchi atahitaji kadi mbili tu (passport, kadi ya Huduma), Kibicho pia alisema kuwa mashine ya bio metric itachukua tu alama za vidole.

Mashine 31,500 viko tayari kufanya kazi kabla ya mradi kufanyika mwezi ujao serikali kwanza itajaribu mradi huo katika kaunti15 na kata ndogo za kaunti 41.

"Katika njia ya kujisajili mwananchi atakuwa akisajiliwa na afisa wa usajili kwa afisi ya chifu,ama kusajiliwa kwa kawaida kabla  ya mtu kuenda kuchukuliwa alama ya vidole,"Alizungumza Kibicho.