Huenda serikali ikapunguza vikwazo ilivyowawekea wananchi wake na kuruhusu shughuli nyingine kurejelewa nchini

waziri
waziri
Serikali inapania kupunguza vikwazo ama masharti makali iliyowekea wananchi wake wakati wa mkutano wa kiusalama utakapofanyika hiyo kesho.

Taarifa zinadai kuwa huenda serikali ikaamua kufungua anga zake na kuruhusu ndege kuanza kuwasili nchini baada ya kupigwa marufuku kama njia ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Hatua ambayo inasemekana kuwa inapania kuinua uchumi wa taifa ambao umedorora kwa muda baada ya shughuli nyingi nchini kusitishwa.

Kenya iliweka vikwazo vya watu kutotoka nje kuanzia saa 7 jioni hadi  saa 5 asubuhi mnamo Machi 27, agizo ambalo lilichukuliwa na serikali kama njia ya kupunguza watu kutangamana katika maeneo mengi.

Agizo hilo aidha lilisongeshwa kwa siku 21 Aprili 25 , siku ambazo zitafikia kikomo Jumamosi  hii.

Kitengo hicho cha Usalama na ambacho huongozwa na rais Kenyatta kitaangazia iwapo serikali itaamuru uchumi wa taifa kufunguliwa ama kutaongeza maambukizi ya virusi hivyo.

Kenya ilikubali mikahawa na hoteli nchini kurejea shughuli zake za kawaidi mnamo Aprili 25 japo kwa kufuata vigezo ambavyo serikali ilikuwa imeweka.

Wakenya wanamatumaini kuwa serikali itapunguza vikwazo vyake ikiwemo kufungua kaunti tano zilizofungwa ambapo usafiri wa ndani na nje ulipigwa marufuku na serikali.

Aidha, huenda hatua ya kusitisha agizo la kuingia kwa nyumba kuanzia saa 7 jioni lisitupiliwe mbali na serikali japo itaamjuru waajiri kufungua biashara zao na kuweka mikakati ya jinsi wafanyakazi wao watakavyofanya kazi, yaani 'return to work plans'.

Kufikia sasa, Kenya imesajili visa 737 vya maambukizi ya corona, watu 40 wakiwa wamefariki huku 281 wakiwa wamepona.

Tanzania ni tishio kwa taifa la Kenya kwani visa ambavyo vimesajili kutoka kaunti za Migori na Kajiado 10 na 19 mtawalia mlitokea katika taifa hilo jirani.