''Huwa namlazimisha mke wangu kuenda kinyozi na sio salon.''Mwanaume ajivunia

hair
hair

Je, unaweza kufurahishwa na mwanaume anayekupimia mambo ya kufanya?

Mwanaume ambaye atakulazimu kuvaa nguo anazopenda, akulazimu kusonga nywele anazo taka na hata pia akuambie ni rangi gani utakayopaka kwenye mdomo wako?

Nafikiru jibu ni La!

Mwanaume mmoja alizungumza na vyombo vya habari na kuwakasirisha wanawake wengi aliposema kuwa, huwa hafurahishwi na tabia ya mke wake kumwomba pesa za kuenda kwenye Salon.

Zaidi ya hayo, mwanaume huyu alisema kuwa, kila mwezi, yeye hununua kila kitu kinachohitajika nyumbani, hulipa kodi ya nyumba na ata karo ya watoto na kwa hivyo,chochote ambacho hajataja huwa hagharamii.

'Zaidi ya hayo, mwanaume huyu alisema kuwa, bibi yake anafaa kutumia pesa zake anazopata akilipwa

kwani  pesa yake ni ya kujikimu maishani.

Vievile,jamaa huyu alikubali kuwa huwa anahakikisha kwamba hakuna pesa yoyote ambayo hutumika kuenda Salon.

Amini usimini, Mwanaume huyu alisema kuwa, huwa haendi kwenye duka kuu pamoja na mke wake na mara kwa mara humuachia mke wake shilingi 300,pesa ya matumizi ya siku hiyo na endapo anataka kufanya mambo mengine basi itabidi agharamike mwenyewe.

Vilevile, mwanaume huyu alisema kuwa, hakuna siku mke wake huwa na nywele ndefu ama kucha ndefu kwani yeye mwenyewe hawezi gharamia bili zile.

Je mnafikiri wanaume wanafaa kugharamia mambo yote ya mke wake?