Ibada ya wafu ya muigizaji Pretty Mutave kufanyika hapo kesho huku mazishi yakiwa ni ya Jumamosi

Muigizaji Pretty Mutave ambaye alifahamika sana kupitia kwa kipindi cha Maza,Aziza,Moyo na miongoni mwa vipindi vingine atazikwa nyumbani kwao Kibwezi kaunti ya Makueni mnamo Jumamosi wiki hii.

Duru za habari ziliarufu kuwa Mutave aliaga dunia alipokuwa anapelekwa hospitali huku akiwa mgonjwa tangu Machi mwaka huu.

Ibada ya wafu ya mwendazake Mutave itafanyika hapo kesho katika eneo la Swahilipot kaunti ya Mombasa ambapo watakao hudhuria watavalia mavazi ya rangi nyeupe na nyekundu, ibada hiyo itaanza saa kumi jioni hadi saa kumi na mbili jioni.

Ujumbe kutoka kwa kamati ambayo inatayarisha mazishi yake ilisoma hivi;

"Mwili wa mwendazake utasafirishwa ijumaa mbele ya mazishi ya jumamosi, kwa mpangilio wa kusafiri kila mmoja wetu anapaswa kujiandaa kwa mapema, tukingoja uamuzi wa jamaa zake ili tuweze kuwajiza mambo na usafiri."

Mwendazake aliaga dunia mnamo Septemba,15, huu mashabiki,marafiki wakituma risala za rmbirambi.

Mungu na azidi kuilaza roho yake mahali pema peponi.