Ida Odinga ashutumu visa vya ufisadi vinavyoendelea nchini

Ida Odinga
Ida Odinga
Mkewe kiongozi wa ODM Raila Odinga, Ida Odinga amejiunga na viongozi wengine nchini kushutumu visa vya ufisadi ambavyo vimekithiri.

Akizungumza katika eneo la Ang’urai kaunti ndogo ya Teso kaskazini kaunti ya Busia wakati wa maadhimisho ya siku ya akina mama duniani, Bi Odinga amewataka wale ambao wamehusika na ufisadi kurejesha mali ambayo wameiba na kujiuzulu nyadhifa zao.

Kwingineko
Mbunge wa Voi Jones Mlolwa ameapa kuendelea kuishinikiza tume ya TSC kuajiri walimu zaidi katika kaunti ya Taita Taveta,akisema idadi ya walimu kaunti hiyo ni ya chini mno ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi.
Mlolwa anasema kinyume na ripoti ya TSC inayoonyesha kuwa kaunti hiyo ina walimu wa kutosha, wanafunzi wengi wameendelea kusalia bila walimu na hivyo kuchangia kudorora kwa kiwango cha elimu.
Kwingineko
Mbunge wa lugari ayub savula ametishia kuupeleka mswada bungeni kumng'atua afisini mwenyekiti wa tume ya kuajiri walimu tsc bi nancy macharia kwa kufanya kazi bila kuzingatia matakwa ya washika dau

Savula amesema macharia amedinda kuwasikiza viongozi kuhusu swala la uhamisho wa walimu almaarufu delocalization ambalo limeathiri uthabiti katika idara ya elimu.

Kwingineko

Kuna umuhimu wa kujumuisha elimu ya uongozi hususan wa wanawake katika mtaala wa elimu nchini ili kuwawezesha wanawake na viongozi chipukizi kuchukua nafasi kuu za uongozi nchini.

Mtaalamu wa uongozi (governance) na demokrasia Christopher Musyoka anasema, ukosefu wa hamasisho na elimu ya uongozi ndio sababu kuu ya wanawake wengi kufeli kuwania au kushinda nafasi za kisiasa.