IEBC yatangaza upya maombi ya kujaza nafasi ya Chiloba

MAKAMISHNA WA IEBC
MAKAMISHNA WA IEBC
Tume ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imetangaza upya nafasi ya kujaza wadhifa wa afisa mkuu mtendaji na katibu wa tume hiyo.

Kupita tangazo katika magazeti siku ya Jumanne, IEBC pia imetowa wito kwa wale waliokuwa tayari wametuma maombi ya kutaka nafasihiyo awali kutuma maombi upya.

Siku ya mwisho ya kutuma maombi ni Jumatatu 3, 2019.

Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya tume hiyo kumpiga kalamu Ezra Chiloba ambaye alikuwa tayari anatumikia marufuku tangu Aprili 2018.

Chiloba alifutwa kazi mwezi Septemba mwaka uliyopita baada ya ripoti ya uhasibu kuhusu matumizi ya pesa za tume hiyo kuonyesha ubadhirifu wa fedha kutokana na ukiukaji wa kanunizi za utoaji zabuni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Mwezi Machi Jaji wa mahakama ya Leba Hellen Wasilwa alitoa agizo la muda kuzuia zoezi la kutafuta mrithi wa Chiloba kufuatia ombi la Henry Mutundu aliyepinga zoezi hilo.

Mutundu alidai kuwa zoezi la kuajiri afisa mkuu mtendaji mpya lilikuwa likifanywa kinyume na sheria na halikuwa na uazi na uajibikaji kama inavyotakikana kisheria.

Tume ya IEBC imekuwa ikihudumu na makamishna watatu pekee, Mwenyekiti Wafula Chebukati, Kamishna Boya Molu na Abdi Guliye.