Ilikuaje:Kukosa baba maishani ni kidonda rohoni mwangu-Martin Githinji

Leo ikiwa ni siku ya wapendanao Martin Githinji na mkewe christine lwanga walichukuwa fursa ya kuja kwenye studio na kueleza safari yao ya ndoa.
"Tulipatana na martin miaka nne iliopita lakini tumekuwa kwa ndoa kwa miaka mbili, na tumebarikiwa na mtoto mmoja

Wakati tulipokuwa tunachumbiana sikuwa nataka mambo na wanaume kwa maana nilikuwa nimeumizwa na mpenzi wangu wa kitambo." Alieleza Christine.

Martin ni muigizaji humu njini na amefahamika sana katika uigizaji wake kwa onyesho la 'Sue na Johnnie' katika kipindi hicho anafahamika sana kama Jonnie.

Christine alichukuwa fursa na kueleza jinsi baba yake mzazi na mama yake walitofautiana na kuachana akiwa na umri mdogo sana.

"Baada ya kufikisha mwaka mmoja mama yangu na baba walitofautiana baba akatoka Kenya akaenda Botswana kufanya kazi

Baba yangu alikuwa mwananchi wa nchi ya Uganda, baada ya muda walikubaliana wanilee pamoja." Alisema Christine.

Martin aliweka wazi kuwa alipeleka mahari yake nchini Uganda ambapo baba ya Christine alikuwa.

"Nilipeleka mahari Uganda, na baba yake alitupa mawaidha ya kuishi kwa ndoa, alipokuwa akiongea na kutupa mawaidha nilihisi kulia

Hii ni kwa sababu niliona upendo wa baba ndani yake." Martin alisimulia.

Christine alikuwa na haya ya kusema,

"Licha ya baba yangu aliniacha nikiwa na umri mdogo, alinisaidia kwa kulipa karo yangu ya shule, na hata nilikuwa nikifunga shule naenda likizo Botwasana kuishi na baba yangu." Alizungumza Christine.

Martin alieleza jinsi baba yake walitengana na mama yake na vile kukosa baba ni kidonda katika roho yake.

"Baba na mama walitengana na baba alipoenda nchini UK alioa na kuanzisha familia yake, hadi sasa hatuna uhusiano mwema na yeye

Kukosa baba maishani mwangu imekuwa kidonda katika roho yangu, nilichukua jukumu la kumlea dada yangu na hado leo hilo jukumu naendeleza

Jina la daddi martoo lilitokana na dadangu kwa sababu nikiwa chuo kikuu niliwadanganya wengi dadangu ni mtoto wangu tangu hapo alianza kuniita daddi Martoo." Alieleza Martin.