Ilikuaje: Pesa zangu za kwanza niliwasaidia wazazi wangu-DJ Shiti

Steven Oduor Dede almaarufu kama Dj Shiti alipata fursa ya kuja kueleza jinsi maisha yake yamekuwa tangu alipoanza uigizaji wake.

Alifahamika sana baada ya kuigiza kipindi cha ' The real house helps of Kawangwere'

"Nilianza uigizaji wangu nilipokuwa mtoto mchanga nilikuwa naiga vile shangazi yangu alikuwa anaongea, binamu zangu walipenda sana

Kila wakati nilikuwa naiga vile watu walikuwa wanaongea, nilipokua mmoja wa binamu zangu alinishauri niwe mcheshi pia muigizaji." Alieleza.

Alianza uigizaji wake wakati wa mazishi ya mzee Ojwang.

"Nilienda kwa mazishi ya mwenda zake Ojwang na mmoja wa marafiki zangu akanikutanisha na Abel Mutua kwa maana wakati huo alikuwa mwandishi wa kipndi cha churchill

Usiku wake alinipigia simu na kuniambia niende katika onyesho la churchill, hapo ndipo nilianza uigizji wangu." Alizungumza shiti.

Shiti ni mtoto wa sita kati ya watoto nane katika familia yao, alieleza jinsi wlivyoteseka baada ya baba yake kustaafu mapema.

"Wazazi wangu hawakujua maisha yatabadilika baada ya baba yangu kustaafu mapema kwa kawaida tulikuwa tunaishi katika nyumba ya kampuni

Tulitoka katika nyumba hizo na kuanza kutafuta pesa za kujikimu maishani, nilipotoka nyumbani nilipata wazazi wangu hawajalipa kodi ya nyumba na nyumba yao kupelekwa katika Agenti." Alileleza Dj Shiti.

Muigizaji huyo anawaletea watoto wa ndugu zake na pia wadogo zake, amekuwa katika uigizaji kwa muda sasa huku akisema pesa za kwanza alizopata alisaidia kuboresha maisha ya wazazi wake.

Amesomea 'public relation' na hajaweza kumaliza kusomea shahada hiyo kwa sababu ya ukosefu wa pesa

"Pesa ambazo nilipata za kwanza niliwasaidia wazazi wangu na kuboresha maisha yao." Alisema Shiti.