Ilikuaje: Benta Akinyi aeleza jinsi alivyo mwagiliwa asidi na mpenzi wake

Benta Akinyi ni mwanamke ambaye alilelewa katika kijiji cha Oyugi, mama yake aliweza kuolewa na mume wa pili akiwa bado mchang. Kkwa bahati mbaya mama yake aliweza kuaga dunia bila ya kuwaambiwa kuwa huyo baba yao alikuwa baba wa kambo.

Kwa muda usiokuwa mrefu baba yake aliweza kuaga dunia na kisha wakafukuzwa kwa na wajomba wao kwa maana hawakuwa wa baba yao bali mama yake aliolewa na wao.

"Baada ya baba kufariki tulifukuzwa nyumbani kisha tukaenda kwa mjomba mmoja ambapo maisha hayakuwa rahisi katika maeneo hayo,

"Tuliweza kuteswa na watoto wa mjomba wangu, walikuwa wanatupea bhangi ili tuvute na kisha tunapo lala, kesho tukiamka tunajipata hatuna nguo zetu za ndani,

"Mjomba wangu akijaribu kututetea shangazi yangu anamuuliza kama tumekuwa mke wake," Alisimulia Benta.

Baada ya muda usiokuwa mrefu ndugu zake wawili waliweza kupelekwa baroni Benta akiwa na miaka tisa, kwa madai kuwa walikuwa wanauza na kuvuta bhangi.

Waliweza kuachiliwa baada ya mashtaka, ndipo wanakijiji waliweza kuwambia waweze kutoka katika kijiji hicho kwa maana watapata matesa mengi wakiendelea kuishi hapo.

Mwanaume ambaye alimumwagia asidi aliweza mtongoza kisha akakubali na kumwambia shida na masaibu ambayo alikuwa amepitia awali.

"Niliweza kukaa na Felix kwa muda wa wiki mbili ,kisha nikamdanganya kuwa nina mjombo ambaye anaishi Eldoret, alinipa nauli ya 300 nikaenda Eldoret.

"Nilipofika Eldoret  nilifanya kazi ya kuosha vyombo katika hoteli moja maeneo hayo, ambapo nilikuwa nalipwa shillingi sabini na kisha nikakusanya pesa hizo nakaenda Nairobi," Alieleza Akinyi.

Akinyi alikuwa na umri wa miaka 13 alipoenda Nairobi, aliweza enda nyumbani ya watoto mayatima ya Mama Ngina, kisha wakamwambia wanachukua watoto wadogo.

Walimuandikia barua ili aweze kuenda kupata usaidizi katika kijiji chao cha Oyugi.

"Niliweza kurudi kwa Felix nikamwambia ukweli wote na kisha akasema ni sawa, aliweza kunielewa,

"Niliweza kumdanganya tena na nikarudi tena Eldoret, nikakosa kupata usaidizi wowote, niliamua kuenda kanisani ndipo niliweza kupatana na askofu kisha kunipa 30,000 za karo na karo yenyewe ilikuwa shillingi 22,000,"Alisema Akinyi.

Aliweza kupelekea Felix pesa hizo na kisha kumpeleka shule kama mzazi wake, baada ya miaka 4 aliweza kuamua kuenda kuwaambia walimu ukweli wa maisha yake.

Alipoamua kumwambia Felix kuwa hawezi kumuona kama mpenzi wake aliweza kukataa na kisha kuamua njama ya kumuua.

"Aliweza kunimwagia asidi kwenye shingo, kisogo na kwa mgongo nikiwa na miaka 16 hii ni baada ya kumuambia siwezi kuwa mpenzi wake,

"Nilikuwa barabarani na sare za shule na watu walipoona kitendo hicho waliweza kunipeleka hospitali, nilikuwa nafunga shule naenda tu kuishi na Felix na kuwa na uhusiano wa ngono na yeye,"Alizungumza Akinyi

Mwanamke huyo aliweza kuja Nairobi baada ya kukamilisha shule ya upili, ndipo aliweza kupatana na mwanaume tu ambaye alimpenda kisha kuanza kumtesa, kumpiga na kumuita maji mengi baada ya kupata watoto wengi.

"Nilipatana na mwanaume ambaye alikuwa anaitwa Omuya Wanjiru, kisha nikamueleza masaibu ambayo nimepitia na kunipenda,

"Baada ya muda mfupi aliweza kuuza shamba kwa millioni tatu na nikabadilisha maisha yake kisha nikamfunza mambo mengi yenye hakuwa anajua,"Aliongea Benta.

Kwa maelezo zaidi skiza Audio ifuatayo: