ILIKUAJE: Eric Omondi alitumia fedha zangu kujijenga - Madini Classic

madini classic
madini classic
Msanii John Philip Ouma almaarufu, Madini Classic, kutoka Migori kaunti aligonga vichwa vya habari wiki iliyopita baada ya kufichua kuwa mcheshi maarufu, Eric Omondi alimtapeli fedha.

Kulingana naye, Omondi naye walikuwa wafanye mipango ya kujenga taaluma yake ya usanii na kufanikisha hilo, alikuwa ampatie shilingi 60,000.

Alieleza,

Juzi hizi wiki mbili nimekuwa nikiongelewa sana story yangu na Eric Omondi na watu wanasema nimemtelekeza mtoto wangu, na pia kuna msanii niliibia fedha.

Eric ni comedian mzuri sana na kipaji kweli na kwenye entertainment ili u grow lazima ushikane na watu kama wale. Aliponifuata Instagram nikamuomba usaidizi fulani akaniambia tukutane.

Tulikutana mara kama tano na akasema kwa sababu yeye ni president wa ucheshi lazima tungefanya introduction kubwa na angehitaji 60,000 ili apate magari na pikipiki.

Madini Classic anasema alibidi aambie management yake wawekeze kwa ile idea na hakujua kumbe Eric Omondi alikuwa anatumia zile fedha kwa manufaa yake.

Aliongeza kuwa Eric Omondi alionesha lile gwaride kwa mtandao wake wa Youtube bila ruhusa yake, isitoshe pia alikuwa anauza bidhaa vya kampuni nyingine.

Licha ya hayo alipomuongelesha, Eric Omondi hakutaka kuzungumza naye kwa miezi miwili na mabosi wake na hapo anasema amejifunza kuwa kuna watu hawatakii wengine mema.

Na je licha ya muziki ni lipi lingine hufanya?

Ndugu zangu alifariki akaniwachia watoto watano na pia watoto wa dadangu pia ni mimi huwalea baada ya kifo chake. Halafu pia nina wazazi wakongwe ambao wanahitaji usaidizi.

Zile fedha zilinikera sana kwani hata shilingi hamsini pia ni kubwa kwangu, isitoshe management pia tulikosana nao.