Ilikuaje: Gladys Boss Shollei afichua siri ya ndoa yake ya miaka 25

Mwakilishi wa kina mama kaunti ya Uasin Gishu, Gladys Boss Shollei ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni.

Gladys Shollei alizungumzia maneno mengi kuanzia jinsi alivyoingia katika ulingo wa kisiasa, kesi zilizomkumba na pia siri ya ndoa yake.

Shollei alikuwa amekumbwa na kesi ya ufisadi hapo awali ambapo alikuwa amekisiwa kutomia vizuri fedha za korti takriban millioni mia tatu wakati alipokuwa msajili mkuu wa mahakama.

Hizo kesi walikuwa wameweka juu yangu zilikuwa za uwongo na hata kesi iliondolewa na nafurahi wakaazi wangu wa Uasin Gishu walijionea ukweli. Alisema Shollei.

Lakini aliwezaje kuhakikisha kuwa kesi zake hazikuleta madhara katika familia yake haswa wanawe?

Nilikuwa na familia yangu kama wasaidizi wangu, mume wangu na marafiki ambao walinishikilia sana. 

Bahati ni kuwa watoto wangu walikuwa katika shule ya kifaransa na kule kuna wazungu ambao hawashughuliki sana. Kitu nilikuwa nafanya nilikuwa na hakikisha kuwa nawaeleza, nikienda kortini naenda nao ili waweze kuelewa.

Watoto wangu walisoma kesi zangu kutoka mwanzo hadi mwisho, shida ni familia wakiskia maneno kutoka nje na sio kutoka kwako.

Lakini je aliingia aje katika ulingo wa siasa?

Sikutarajia kuwa mwanasiasa lakini wakati niliondoka kazini, mimi ni mkulima pia na nikiwa nyumbani ukikutana na watu wanakuambia wameshindwa kulipa nyumba au karo.

Nikaangalia shida ya watu wangu na nikasema maneno ya bei ya mahindi lazima tubadilishe sheria kwani watu hubadilisha sheria kupitia siasa.

Shollei alisema kuwa uhusiano wake na gavana wa Uasin Gishu, Jackson Mandago umeimarika kwani yeye humshirikisha katika miradi yake yote.

Mwanasiasa huyo amefanikiwa na watoto wanne katika ndoa ya miaka ishirini na mitano, na anasema kuwa siri ya ndoa ni kutafuta shida kati yenyu wawili na kutafuta suluhu.

Vile unakuja kazini kila siku unapata challenge you find a solution and work on it.

Je ni kitu gani humuudhi sana kumhusu mumewe?

Akija na wageni nyumbani bila notice, hilo huniudhi.