guardianangel160115

Ilikuaje: Guardian Angel aeleza jinsi alivyoteseka baada ya kukataliwa na babake

Mwanamziki Guardian Angel almaarufu Audiphaxad Peter amelelewa na mama peke yake kwa maana aliweza kukataliwa na baba yake akiwa bado hajazaliwa.

Ni mkristo ambaye amepitia mengi kisha kuja kuwa mwanamziki maarufu wa nyimbi za injili.

Guardian amekuwa akiimba kwa miaka nane mwaka wa 2017 ndivyo alivyojulikana mzuri na mashabiki wake.

Offences your favourite sportsmen have ever been charged with

“Ilifika kiwango mpaka nikasikia kuacha kuimba nyimbo za injili kwa maana nilikuwa naona nyimbo hizo zingine ziko na mashabiki wengi kuliko za injili hasahasa zangu.

“Nilikuwa nimepanga niimbe wimbo wangu wa mwisho kisha niwache lakini na mshukuru mungu hakuniacha,” Alisimulia Angel.

guardian angel
                 Mwanamziki guardian angel

Mwanamuziki huyo aliweza kuachwa na mamayake ili aje kutafuta kazi Nairobi, ndipo aliweza kuachwa na nyanya yake.

Alieleza kuwa maisha kwake haya kuwa rahisi kwa maana babu yake alikuwa ni wa kambo kwa hivyo aliweza kusisitiza apelekwe kwa baba yake aliye pachika mamake mimba.

Guardian alitoroka nyumbani kwa sababu ya mateso akaenda kuishi mitaani.

“Nilienda kuishi mitaani nikakua chokora yaani kijana wa mtaani katika eneo la western Butere kwa mwaka mmoja ndipo mamangu alipokuja kutoka Nairobi kunichukua,” Guardian alielezea.

Aliweza kuongezea na kusema kuwa ni yeye alikuwa kijana wa mtaani wa kwanza katika eneo hilo la Butere.

guardianangelartworkforradiojambo
Guardian Angel alijiunga na Massawe Japanni

Walipokuja Nairobi na mamake kazi iliisha na kuanza kuteseka tena ndipo alipo rudi mitaani tena hili kujikimu, alikaa mitaani kwa miaka miwili.

Heartbreaking: Body of missing Nation employee found at city mortuary

“Nilikuwa nishaa zoea maisha ya mitaani kwa hivyo nilitoka nyumbani nikaenda mitaani tena lakini mamangu hakujua ama nimerudi mitaani tena,” Aliongea Guardian.

Mama yake aliweza kuongea na babake mzazi wa Angel akiwa na miaka kumi ilhali hakuwasaidia na chochote.

Baada ya miaka miwili rais Uhuru Kenyatta kuamuru vijana wote ambao wako mitaani washikwe na kupelekwa shuleni mwa mayatima.

“Baada ya rais kuamuru tupelekwe shuleni mimi nilienda baroni kwa miezi miwili kisha nikapelekwa ‘Approved school’ baada ya hapo tuliweza kuambiwa ambao wanajua kwao wapelekane ili kuona jamii zao,” Alisema Angel.

Baada ya mwana mziki huyo kutoka shuleni, waliweza kuhama Kibera kisha wakaenda Mwiki na mamake ambapo maisha yalikuwa magumu zaidi.

Exclusive: Gospel singer Pitson reveals his valentines day plans

“Niliokoka nikiwa jela na kutoka nikue mndogo mama yangu alikuwa mkristo, huwa naomba sana katika maisha yangu,” Alizungumza Angel.

Angel ni mwanamziki ambaye hajaoa, aliweza kusema kuwa wana mziki wengi huwa wanaimba tu ili waweze kuonekana lakini si kusambaza injili ya yesu.

Baada ya kutoka ‘approved school’ Guardian alirudi nyumbani ili aweze kukamilisha masomo yake. Alipofika kidato cha tatu aliweza kutoa wimbo wake wa kwanza ambao unaitw ‘Amaizing grace’.

 

 

 

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments