Ilikuaje: Johnson Mwakazi aelezea alivyojipata katika mtego wa sinema za ngono

Aliyekuwa mtangazaji wa Citizen, Johnson Mwakazi ndiye aliyekuwa mgeni wetu leo katika kitengo cha Ilikuwaje naye Massawe Japanni.

Moja wapo ya mambo aliyoangazia katika mazungumzo yake ni jinsi alivyojipata ametekwa katika sinema za ngono almaarufu, Pornography.

Kulingana na Mwakazi, alijipata ameingilia maneno ya sinema za ngono akiwa katika darasa la nane baada ya rafikiye kumshawishi amlipie sinema bila yeye kujua.

Alielezea kuwa pindi tu alipoingia mle ndani alipata watu wa aina mbali mbali wamekusanyika wakitizama sinema hizo za ngono, na hilo lilibadilisha maisha yake.

Aliporudi nyumbani siku hiyo, alishindwa kumuangalia mamake mzazi kwani alikuwa amejawa na aibu chungu nzima.

Nilikuwa darasa la nane na mwenzangu aliniambia kuna kipindi atanilipia na sikuwa najua. Pale kuingia nikaingia kwenye mtego, nilipopata hela nikatafuta mwenzangu na nikamlipia. Alisimulia Mwakazi.

Aliongeza, Siku ya kwanza niliporudi nyumbani nilikuwa naogopa kumwangalia mamangu kwani hakuna mwenye alituzuia.

Nilipoingia kidato cha kwanza mwalimu mmoja alisimama kwa darasa na kusema kuwa kutizama sinema za ngono ni dhambi na hapo nikawacha kabisa. Kama umekuwa ukitizima hayo maneno kimbia.

Ili aweze kujizuia kutizama zile sinema, Mwakazi alijizuia kutizama televisheni kwa mda wa takriban miezi tano.

Baada ya kupitia hayo yote, Mwakazi aliamua kumpa mungu maisha yake katika mwaka wa 2005, na ingawa alifanya kama mzaha, anakiri maisha yake yamebadilika.

Nilikuwa shule ya upili ya Jamhuri na niliweza kuokoka kwa sababu siku moja mhubiri aliuliza nani anataka kumpokea kristo na wenzangu walipoenda pale mbele, nikaamua kuwafuata tu.

Sikuwa najua mambo ya wokovu lakini mwalimu wangu mmoja ambaye ni mwalimu aliweze kunikuza kiroho. Alisema Mwakazi.

Mwakazi ni kitinda mimba katika familia ya watoto saba.

Mamake mzazi alifariki mwaka wa 2006 na yeye na ndugu zake walichukuliwa na baba wa kambo kutoka maeneo ya Taita, ambaye alikubali kuwalea kama wana wake.