Ilikuaje: Millicent Omanga afichua sababu za kukataa kuwa naibu wa Mike Sonko

Millicent Omanga ni mke wa mume mmoja na mama wa watoto wawili- mvulana wa miaka 12 na msichana 8.

Si mke tu wala mama pia ni mwanasiasa ambaye ameteuliwa kama seneta wa kaunti ya Nairobi.

Alipoanza siasa zilizopita aliweza kujipa jina 'msupa na kazi'. Alisema kuwa msupa si umbo wala urembo wake bali msupa ni kazi na kutekeleza majukumu ya wananchi.

Pia Seneta huyo alisema kuwa Sonko ni rafiki wake wa karibu mno ambaye anapenda kutekeleza mahitaji ya wananchi.

"Sonko ni rafiki wa karibu na anapenda kuwasaidia wananchi sana, na pia gavana wetu hapendi ufisadi anaposimama kupinga ufisadi watu wanamuona ni mbaya lakini hawajui ukweli kuwa sonko ni kiongozi wa watu,"

"Pia analinda mali ya mwananchi na ana utu na ni mzuri na pia anajali maslahi ya watu wengi, hata huko vijijini watu wanasema maisha yao yamebadilika kwa sababu ya gavana wetu kwa hivyo si kukataa ombi la Sonko na nia ingine bali kutaka kumaliza kazi yangu,"

"Gavana Sonko pia anaweza kuwa gavana na naibu kwa maana ni kiongozi ambaye ana maendeleo," Alisema Millicent.

Aliweza kusema kuwa kazi ya seneta mteuliwa ni sawa na ya seneta kwa maana wanafanya kazi sawa na wala sikukaa bure na kukula mali ya umma kama vile watu wengi wanaona.

"Tuko katika ofisi ili kutengeneza sheria zitakazo linda wananchi bali si kukula mali ya umma," Omanga alisisitiza.

Pia aliweza kuelezea kuwa wakati ambao waliweza kurushiana maneno na Babu Owino haikuwa vita bali vifaranga wa Babu Owino ndio waliweza kuingia kwenye mtandao na kumtusi Omanga.

Licha ya hayo yote seneta mteuliwa na Babu ni marafiki.