Ilikuaje: Mr Seed aeleza kwanini waliweza kukosana na msanii Bahati

Moses Tarus Omondi almaarufu Mr Seed ni mwanamziki ambaye alianza usanii wake akiwa shule ya upili.

Mwezi mmoja uliopita Mr Seed aliweza kukosana na msanii ambaye wamekuwa na yeye kwa miaka 16 kwa sababu kadhaa.

Mwanamziki huyo alisema kuwa aliweza kutoa wimbo wake wa kwanza akiwa katika kidato cha pili.

Mr Seed ndio aliweza kumkaribisha mwanamziki Bahati katika sekta ya usanii kisha wakaweza kutoa wimbo wa 'wangu' wakiwa pamoja.

Baada ya kutoa wimbo huo mwanamziki huyo aliweza kurudi shule kumaliza masomo yake ya shule ya upili.

Wasanii hao waliweza kushirikiana kwa mambo ya kiusanii, lakini mnamo tarehe 31 Desemba mwaka jana wasanii hao waliweza kukosana kwa ukosefu wa nidhamu na heshima.

Aliweza kusema kwa kuwa hana ugomvi wowote na msanii Bahati wanaeza kufanya kazi na yeye.

Mwanamziki huyo alikasirika tena sana wakati wa kisa hicho kilicho sababishwa na Bahati kwa maana aliona mke wake anasumbuliwa sana na ilhali alikuwa na ujauzito.