ILIKUAJE: Sababu yangu ya kumficha baba mtoto - Jackie Vike (Awinja)

awinja
awinja
Msanii wa kipindi cha Papa Shirandula, Jackie Vike, almaarufu Awinja leo amefunguka kuhusu mbona yeye huificha familia yake ikiwemo baba mtoto na pia mwana wao.

Kinyume na wasanii wenzake ambao wana tabia ya kuchapisha picha za familia zao mitandaoni na pia kuwa na mitandao ya kijamii kwa niaba ya wanao, Awinja hajawahi ona haja ya kufanya lile.

Anasema kuwa yeye huwa na uwoga wa kuchapisha picha za mtoto wake mtandaoni kisha atusiwe kwa sababu ya maumbile au jambo lingine. Anakiri kuwa pia hataki kumpa mwanawe presha ya maisha na anapendelea mtoto akuwe kama wana wenzake bila kujali.

Kama mzazi unajua mtoto ni kitu cha maana na sababu yeye hayuko mtandaoni ni kuwa watu wanajua chenye nafanya na mimi huogopa nikaweka mtoto wangu mtandaoni kisha watu waanze kumpiga vita hapo ndipo naweza kasirika. Alisema Awinja.

Aliongeza,

Mtoto wacha awe mtoto hata akitaka kucheza na mchanga aanguke kwa mitaro.

Je baba mtoto yuko?

Yuko baba watoto na kama mimi yeye sio mtu wa kuonekana kwani yeye hufanya kazi za uzalishaji vipindi (production).

Alipoulizwa kuhusu mipango ya ndoa alisema kuwa yeye alianza na njia tofauti ya kupata mtoto na sasa watatongozana kisha labda afanye harusi au pia akose.

Mzaliwa huyo wa Eastleigh pia alizungumzia kuhusu uwoga au shida aliyokuwa nayo tangia akiwa mdogo. Kulingana na Awinja, alikuwa anaamini kuwa taya yake (Jaw) ni kama ya mwanaume na kuwa haipendezi na hapo kumfanya kutopiga picha ambayo inaonesha uso wake kwa karibu.

Ukiwa mkubwa chenye watu hukuambia ndio utaishi nacho na mimi kwa mfano taya zangu zaonekana sana na watu walikuwa wanasema zinakaa za mwanaume mara zinafanana na Kanye West na sikuwa napiga picha ya karibu.

Baadaye nilifika mahali nikaona mimi ni mjinga kwa kuamini kuwa taya zangu ni mbaya.

Anasema kuwa ilifika mahali na akajikubali kwani hayo ni mambo ambayo hawezi badilisha na ndio maana siku moja alichapisha ujumbe kwa mtandao wa Instagram.