Ilikuaje: Tulikaa na mke wangu kwa miaka 5 bila kupata mtoto - Raila Junior

railajuniorandmasssawe
railajuniorandmasssawe
Raila Junior ni mtoto wa kinara wa ODM Raila Odinga, ni mwana biashara ambaye ana kampuni zake ambaye ni mzalishaji wa kampuni zake.

Akiwa katika mahojiano na Massawe Japanni, alisema kuwa watu wengi huwa wanampa kazi si kwa ajili yeye ni mtoto wa Raila bali kwa sababu wanajua utaalamu wake uko katika kiwango cha juu.

"Watu wanapotupa kazi ili tuwafanyie huwa wanatarajia kazi mzuri si kwa ajili wanajua mimi ni mtoto ama mtu ambaye ametoka kwa familia kubwa,

"Huwa nafanya kazi na kampuni kubwa kwa ajili ya utaalamu wangu na wanajua kuwa uko katika hali ya juu." Alisema Raila Junior.

Raila Junior akiwa katika miaka kumi ndipo aliweza kumuona baba yake mzazi ambaye ni Raila kinara wa chama cha ODM.

"Niliona watu wakiwa wamejaa nyumbani kwa mama yangu hapo ndipo niliweza kumuona babayangu,

"Nilikuwa mtoto mdogo kwa hivyo sikujua ni nini kilichokuwa kinaendelea, huwa napingana au natofautiana na baba yangu kwa mambo ambayo huwa anasema,

"Si kwa sababu simpendi lakini huwa na msimamo wangu, hilo ni jambo la kawaida katika familia." Raila Junior aliongea.

Kwa mara nyingi katika mitandao ya kijamii Raila Junior huwa anatofautiana na babayake, alisema kuwa Raila ni mwanadamu wa kawaida.

"Baba huwa anakasirika wakati jambo linaenda vile halistahili." Aliongea.

Mwanabiashara huyo alisema kuwa wakati walipompoteza ndugu yao wa kwanza Fidel Odinga, lilikuwa pigo kubwa kwa familia  kwa sababu alikuwa anawalinda mzuri kama kifungua mimba.

Akiongea katika mahojiano hayo, alisema kuwa waliweza kukaa miaka mitano na mke wake bila kupata mtoto lakini kisha baadaye aliweza kubarikiwa na mtoto mvulana.

"Tulikaa kwa miaka mitano bila kupata mtoto, sikuweza kumsukuma bibi yangu kwa maana kila mtu alikuwa anasukumwa nje na marafiki,

"Baadaye na mshukuru Mungu kwa sababu aliweza kutubariki na mtoto mvulana," Alisimulia Raila Jumior.

Alisema kuwa hana nia yeyote ya kisiasa kwa sasa labda katika maisha ya baadaye kwa maana kwa sasa anakuza biashara na kampuni zake.

Raila Junior alisema kuwa yeye huwa anakula mahali popote yaani hoteli zozote, na kutozungumzia ama huwa na walinzi.

"Mimi huwa nakula mahali popote hotelini Mombasa hata hapa mjini Nairobi, kwa sasa siwezi ongelelea ama niko na alinzi kwa sababu ya usalama wangu," Raila Junior alisema.