ILIKUAJE: Wazazi walijua mimi ni mwanamziki baada ya wimbo kutamba - Aslay

Aslay, 25, msanii maarufu kutoka Tanzania ambaye alitambulika kupitia bendi ya Yamoto ndiye aliyekuwa mgeni wetu leo katika kitengo cha Ilikuaje.

Kama kawaida swali la kwanza ni je mbona wakatengana na wenzake kina Mbosso na kila mmoja kwenda kivyake.

"Kila mtu aliona ni wakati wa kufanya kazi kivyake kwa hivyo pesa ndizo zilifanya tutengane. Kwa mfano ukiwa pekee yako unapata pesa nyingi kuliko ukiwa kwa bendi." 

Je alizaliwa wapi?

Nimezaliwa Dar es saalam nimeanza mziki mwaka wa 2013 na baada ya miaka mitatu kabla kuungana na Yamoto Band. Wazazi wangu hawakuwa wanajua mimi ni msanii na walijua mimi ni mwanamziki wakati wimbo wangu umevuma.

Je yeye hupambana aje na watu walio na tabia ya kutusi au kukejeli watu kwa mitandao ya kijamii?

Ukishakuwa maarufu vitu kama hizo huviweki mbele na ukiwa roho nyepesi utawaachia muziki, kwangu naona kama jambo la kawaida sana.

Vitu ambavyo huniudhi ni kama mashabiki kutafsiri mambo yenye naimba, au nimeposti kitu. Lakini ni vitu vinatupa nguvu za kufanya kazi. 

Maisha ya usanii yamekuwaje?

Nikianza muziki watu waliona nikiwa mdogo lakini namshukuru mungu kwani nilivuka vikwazo hivyo.

Aslay alitupilia mbali pendekezo la kujiunga na kundi la Wasafi linalo ongozwa na msanii Diamond Platnumz akidai kuwa lengo lake ni kukuza vipaji.

Nahitaji kufungua label yangu sitaki kuwa chini ya label kwani nia yangu ni kuinua wasanii wengine.