Ilikuaje: Willy Paul aeleza kwanini akaimba nyimbo za kimapenzi

Willy Paul ni msanii ambaye anajulikana sana katika nchi ya kenya, ni kitinda mimba katika familia yao, alilelewa katika maeneo ya Mathare kaunti ya Nairobi.

Msanii huyo aliweza kusema anaamini katika maneno ya mapenzi, kwa yale amepitia na kusema kuwa mapenzi ya kweli aliweza kuona mara ya mwisho na mama na baba yake.

"Mapenzi ya ukweli niliona mwisho na mama na baba yangu na sipendi mapenzi na siamini mapenzi, kwa maana wanawake wanamambo mengi sana,"Alieleza Willy Paul.

Alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha msanii huyo yuko tayari na hivi karibuni mashabiki wake wata usikia.

Mwanamziki huyo ameweza kuimba nyimbo nyingi ambazo zinawapendeza mashabiki wake na zingine amabazo mashabiki wake wanazikejeli.

Alieleza kuwa gavana wa Mombasa ni rafiki yake na wanafanya biashara pamoja ilhali hana mafikra ya kuwa mwanasiasa.

"Gavana Joho ni rafiki yangu na pia kuna biashara ambazo tunafanya mimi na yeye," Willy alizungumza.