Ilikuaje:Nilikataliwa na familia yangu kwa maana sikuwa na baba

Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye country man, ambapo alilelewa bila baba na alikataliwa, na jamii sana baada ya kuachwa na mama yake akiwa na umri wa chini alianza kuuza majani chai.
"Nilikuwa naenda wiki mbili shuleni na wiki zingine mbili naenda kutafuta pesa, nilikuwa nalipwa shillingi mbili, nilitaani maisha ya watu wenye hawana mwelekeo

Nilianza wizi nikiwa darasa la nane, nilienda shule ya upili nilipokuwa naenda shule jamaa zangu walinifanyia matayarisho ya shillingi 21 nilipofika shulleni nilianza kuiba mpaka nikafukuzwa

Nilienda kuzurura Nakuru wakati mmoja kwa maana nilikuwa na machungu ya kukataliwa na familia yangu, tulimvamia mjomba wangu na hata kumnyang'anya pesa tukapelekwa polisi

Kesi yetu iliposikizwa nyanya yangu alinitetea na hata kunifukuza na kuniambia niende kabisa." Alieleza Country Man.

Baada ya Muda Country Man alikuja Nairobu ambapao aliendelea na kazi yake ya wizi na hata kukamatwa na polisi na kupata kifungo cha miaka mitatu kwa kufanya uhalifu.

Alipotoka jela kwa mara ya kwanza alirudi tena baada ya kukata mtu mwingine bali hakupenda kufanya hayo kwa maana alikuwa na maumivu na machungu kwenye moyo wake kwa kuachwa.

Baada ya kutoka jela Country Man alianza kuchota maji huku akilipwa, licha yake ya kuchota maji alikuwa na chawa ambazo watu walikuwa wakiziona hata akianika nguo zake.

Baada ya muda Aliokoka na kuanza kubadilisha maisha ya vijana wengi.

Kwa mengi zaidi tembelea youtube yetu.