Ilikuaje: Hart the band wamerejea na ubaya

Je,Unawakumbuka Hart the band kweli?

Hii leo kwenye kipindi cha ilikuwaje tumezugumza na moja kati ya bendi iliyotetemesha ulimwengu wa nyimbo hapa nchini Kenya mwaka 2014, Hart The Band.

Kikundi hiki kilichoanzisha makali yao mwaka 2013 kimerejea mwaka huu na albamu ya mpya, 'Made in Streets'.

Hart the band ni kikundi cha vijana watu, Kenchz Muya,Skoko  pamoja na Mordecai.

Kila mmoja wao ana jukumu lake kuhakikisha kuwa bendi yao inafanikiwa kufanya kweli.

Kenchz ni mpiga guitaa huku Mordecai na Skoko wakiwa waibaji na wakariri wa mashairi.

Wakali hawa walipatana wakifanya uigizaji wa vitabu vya shule za upili mwaka 2013 na walifanya kazi kwa pamoja miaka miwili kwenye streets.

 "Sisi tulikuwa tunaigiza vitabu kama Utengano kwa wanafunzi wa high school hadi pale tulipofika Kenya theatre ambapo tulipatana na management yetu ikatusponsor. Tuliamua kubadilisha swala na kuchukua uimbaji badala ya uigizaji baada ya kuangazia maswala ya kifedha pamoja na uchovu pia."

Mwaka huu umekuja na mafanikio mengi sana kwa hart the band kwani wameachilia vitu moto moto baada ya kurejea.

"Tunajua tumekuwa nje ya sanaa hii kwa muda wa miaka mitatu sasa. Tumekuwa tukiandika nyimbo na tumefanikiwa kuandika nyimbo sitini lakini tumechoose nyimbo 13 pekee zenye zimeweza kwa hio Ilikuwaje: Hart the band wamerejea na ubaya saiAlbum mpya ya made in streets'.

Hart the band kwa sasa ni wazazi wengi wao hivyo wanaelewa changamoto wanazopitia wazazi wote katika safari ya kuwalea wanao ila wamewashauri wazazi wasisite kuwapea wanao motish kuhusiana na talanta zao.
"Mimi sikupata usaidizi kutoka kwa wazazi wangu nikiwa mdogo lakini nilijikakamua na nkafanya kweli. Baba yangu alinifukuza nikaenda kwa beste yangu alipojua kuwa nilikuwa nafanya muziki," Mordicai alisema.

"Wazazi tafadhali wapeni watoto wadogo uasidizi kwa talanta zao. You never know of kesho."

Pamoja na hayo, Hart the band wamewashauri wanamziki wenzao pia kwa kusema,

"Wewe kama msanii ukipewa kipaza sauti tadhali jaribu utoe ujumbe wa maana kwa wananchi wanaokusikiliza ili watoto pia wasikuwe na matatizo kusilikiliza nyimbo pamoja na wazazi wao."