Ilikuwaje: Mpenzi wangu alinivunja moyo na nikaamua kuwa kahaba - Jane Watiri

jane watiri
jane watiri
Leo studioni tulikuwa na Jane Watiri ambaye alikuwa kahaba kwa miaka saba lakini sasa amegeuza mienendo yake na kuwa mhubiri.

Watiri alifichua kuwa aliingizwa katika biashara ya ukahaba akiwa na umri mchanga na rafikiye wakati alipokosa namna ya maisha.

Hayo yalifanyika baada ya kupachikwa mimba akiwa na umri wa miaka kumi na saba, mimba ambayo baba mtoto aliikata na pia kumtenga.

Rafiki aliyemwezesha kuingilia ukahaba alikuwa amemshinda ki umri kwani alikuwa na miaka 32, takriban mara dufu ya miaka yake Watiri.

Kulingana na Watiri, alifanya ukahaba kwa miaka saba huku akijaribu kuuponya moyo wake baada ya kuvunjwa na mpenzi wake.

Alieleza: Wakati nilijifungua mtoto nikiwa mchanga, baba mtoto alinikataa na nilikimbia Koinange kutafuta riziki na pia kuuponya moyo wangu.

Rafiki yangu mwenye umri mkuu kuniliko alinifunza kazi ya ukahaba nikiwa umri wa miaka 17.

Huyo rafiki yangu aliniambia kuwa atanipeleka kazi na wakati huo mtoto wangu alikuwa na mwaka mmoja unusu. Nilikuwa nampa dawa ya kulala na naenda ukahaba usiku mzima.

Mtoto wangu ilifikia mahali na mwili ukaanza kuzoea zile dawa na hapo mamangu alimkujia na kwenda naye nyumbani.

Hata hivyo, sahizi amebadilika na yeye ni mhubiri. Hata hivyo, Watiri amewashauri watu kuto wahakimu kahaba kwani kuna aina tatu ya ukahaba.

Moja ni ukahaba wa kujitakia, pili ni kahaba ambaye hataki kufanya kazi na anataka fedha na tatu ni kahaba ambaye amevunjwa moyo na mpenzi wake.

Sahizi mimi ni mhubiri baada ya maisha ya ukahaba kwa miaka saba na nilikuwa natumia bangi. Kwa sasa siwezi ambia wasichana watumie bangi kwani haikubaliki hata kwa jamii.

Kuna kahaba mara tatu; Kuna ule wa kujitakia labda hataki kufanya kazi, kuna mwenye anaifanya kwa hiari yake na pia kuna mwenye amevunjwa moyo. Kwa hivyo ukiona kahaba usiwahi wahukumu.

Kazi ya ukahaba ina hatari mbali mbali kwani Watiri aliwahi lala korokoroni kwa mwezi mmoja baada ya kumuongelesha jaji vibaya.

Isitoshe, ashawahi patana na wateja ambao walitaka kumtumia kama dhabihu huku mwingine akitaka kumpiga risasi bila sababu. Lakini kwa bahati nzuri aliponea yote.

Niliwahi shikwa juu ya ukahaba na nikapelekwa kortini na kufungwa mwezi mmoja baada ya kumuongelesha jaji vibaya. Aliniuliza kama nilikuwa nafanya ukahaba nikamjibu 'Kwani unaonaje?'.

Hapo akaniambia niende korokoroni ili nipate adabu kwani asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.

Akizungumzia kuhusu siku aliyoponea kutolewa kama dhabihu alisema.

Nishawahi patana na client akaniambia nimngoje afike up stairs, alirudi akasema miungu yake imekataa nitolewe kama dhabihu. Hapo nikajua kuwa kuna watu hukujia wanadada barabarani na kuwatoa kama dhabahu.

Pia nishawahi shikiwa bunduki Uhuru Highway na mteja wangu saa nane usiku. Jamaa alisema kuwa anajihisi kuniua na kilichoniokoa ni polisi fulani walikuja na hapo nikatoweka.