INDIA: Mashua yazama na kuua watu 12, wengi hawajulikani walipo

india
india

Watu kumi na mbili wafariki na zaidi ya watu 20 kupotea baada ya mashua moja iliyokuwa imewabeba watalii kuzama kwenye   mto mmoja nchini India.

Mashua hii iliyokuwa imewabeba  watu 60, iligongana na jiwe kubwa  ilipokuwa njiani kuelekea kwenye mtaa mufti wa kuzuru.

Kundi la Rescue Team liko katika harakati za kuokoa maisha ya watu hawa.

Mama mmoja aliyenusurika kutokana na ajali hiyo alikuwa na huzuni sana alipozungumza na BBC kwani, mama huyu amefiwa na bwana na mtoto wake katika ajali hiyo.

Zaidi ya hayo,Mama huyu alisema kuwa, ingekuwa heri yeye afe lakini si mtoto wake.

       "I should have died not my baby,"

Ama kwa hakika, kifo hakichagui mkubwa ama mdogo.

Vile vile,Chief Minister wa nchi hiyo, Jogan Mohan Reddy, ametoa amri kuwa safari zote za mashua zisimamishwe wakati huu.

Prime Minister  naye alityuma rambirambi zake kwa familia zilizoathirika kupitia mtandao wa Twitter.

https://twitter.com/narendramodi/status/1173206429722906624?s=20

Wanasheria waliwaambia BBC kuwa, ajali hii ilitokea mahali ambapo kuna msitu na pia hakuna vifaa vya kuzungumza na ndio sababu ilikuwa vigumu sana kuwaokoa wahusika.

Waziri wa usafiri naye alisema kuwa,mashua hii ilikuwa inafanya kazi pasi na kuwa na Leseni ya kusafiri.

BBC