Isome bajeti ya hafla ya Bob. Kwa nini hakutaka wanasiasa katika hafla hiyo ya kumuaga?

Bob_Collymore_Safaricom__1562321064_34850
Bob_Collymore_Safaricom__1562321064_34850
Bob Collymore alikuwa ni kati ya viongozi wapole zaidi na ambao hawana majishauo ya kuonyesha utajiri wao hadharani. Bob alikuwa na mshahara wa takriban milioni 10 kila mwisho wa mwezi. Hafla yake ya kumuaga ingekuwa kubwa zaidi ukizingatia ana cheo kikubwa, ana marafiki wakubwa serikali na zaidi ya hapo alikuwa anaiwakilisha kampuni kubwa afrika mashariki.

Soma hapa:

Katika hafla ya kumuaga, bajeti yake ilikuwa ya wastani kabisa. Katika jamii inayopenda kujishembedua na jinsi tunavyovimiliki utajiri mkubwa, mamlaka, wengi walikusudia hafla kubwa zaidi ya kinyamwezi na ya gharama kubwa. Ila kiongozi huyu hakutaka maonyesho hayo ya utajiri mkubwa katika wasia aliouacha.

Gharama yote ya kuuweka mwili wake sawa katika hifadhi ya maiti ni kiwango ambacho mkenya wa kawaida anaweza akakifikia. Gharama hii inakisiwa kuwa kiwango cha wastani takriban 63,000 kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vilivyohusika katika maandalizi. Uchomwaji wa mwili ulifanyika kwa shilingi 5,000.

Aidha gari iliyobeba mwili kutoka hifadhi ya Lee ikifikia 10,000 bei sawa na gari iliyobeba mwili na kuupeleka Kariokor jumanne.

Hifadhi ya maiti ya Lee iligharimu elfu 18,000 kwa usiku huo mwili ulipumzishwa pale. Jeneza ikiwa ya gharama 20,000.

Soma hapa pia;

Moja kati ya marafiki wa Bob waliomtembelea Kitisuru alifunguka kuwa kiongozi huyu hatutaka kufariki kwake kusherehekewe kwa gharama kubwa.

"Aliweka wazi kuwa mwili wake uchomwe kati ya masaa 24 katika Kariokor na kukataa mpango wowote wa kufanya sherehe kubwa ya mazishi." alisimulia rafiki yake.

Bob alikataa pia uwepo wa wanasiasa katika mazishi yake. Aliitaka familia na marafiki wa karibu peke yake.