Ivlyn Mutua aacha kuimba nyimbo za injili na kuimba za kidunia

Sham Sham si video ya kawaida ya Ivlyn Mutua. Msanii huyo amebadilisha nyimbo zake kutoka kwa injili hadi muziki wa kidunia.

Ivlyn alisema kuwa alifanya uamuzi wa kuwafikia watu ambao hawawezi kuzungumza juu ya Yesu.

"Mimi ni msanii wa kisasa ambaye atakuwa akiimba juu ya kila kitu na si kuhusu Yesu pekee," Ivlyn alisema. Aliendelea kusema kuwa baadhi ya wasikilizaji wake hawajauchukua uamuzi ule vyema na wanamuita majina.

"Wengine wanasema mimi ni mwabudu shetani na kusema kuwa nimerudi nyuma. Lakini ninachukua muda wangu ili watu waelewe ya kwamba hakuna kitu kinachoweza kunitenganisha kutoka kwa Yesu, "Alisema.

"Watu hawakutarajia haya kutoka kwangu lakini nataka waweze kukua nami." Ivlyn alisema kuwa wazazi wake walimuunga mkono alipowaelezea wazo lake. Sham sham ni wimbo wake wa kwanza wa kidunia.

"Sikuwahi dhania kuwa nitakuwa msanii wa kidunia lakini unapoendelea kukua, unapata uwazi zaidi ya yale uliyoyajua kutoka kanisa," alisema.

"Kushirikiana na wasanii wa kidunia ilikuwa vigumu na mtazamo wangu juu yao ulikuwa tofauti kabisa na kile nilichopata baada ya kuingiliana nao.

Yalikuwa mazingira tofauti kwangu. "

soma mengi hapa