Jacque Maribe alamba dili nono baada ya kuitema runinga ya Citizen

Mwanahabari shupavu Jacque Maribe amepata kibarua kipya baada ya kuitema runinga ya Citizen.

Maribe alikatisha mkataba wake na runinga hii hapo awali.

Jacque alianza taaluma ya uanahabari katika kituo cha K24 mwaka wa 2009 baada ya kufuzu chuo kikuu cha Nairobi.

Jina la nyota huyu lilipakwa tope na madai ya kuhusika katika mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Maribe alisaini kumaliza mkataba wake na runinga ya Citizen kile alichokitaja kama "sababu za kibinafsi.

https://www.instagram.com/p/BnCARb8HOnA/

Inaaminika kuwa Maribe amepata kazi badala ambayo inamuweka katika ramani ya umaarufu nchini.

Mrembo huyu sasa anafanya kipindi kinachoruka kupitia 1824 kinachohusisha maswala ya burudani.