Jacque Maribe amjia juu shabiki kisa ombi la dhamana kwa Jowie Irungu

Jowie-Maribe-470x264
Jowie-Maribe-470x264
Jacque Maribe amemjia juu mfuasi katika mtandao wa Insta aliyejaribu kutoa kauli kuhusu kesi inayomuusisha na mauaji.

Maribe ni mshukiwa wa mauaji ya mwanabiashara Monica Kimani.

Mwanadada huyu alijawa na ghadhabu baada ya kauli ya kutoka Jowie Irungu apewe dhamana katika kesi inayomwandama.

Kilichomkasirisha ni kuwa shabiki kwa jina Wambui_glory alipemdekeza apewe dhamana kama Aisha Jumwa na Jacque Maribe.

Aisha Jumwa ana dhamana ya kesi ya mauaji ya mkaazi wa eneo la Ganda , Ngumbo Jola.

Jola alipigwa risasi na kuuawa na mtu asiyejulikana hadi kufikia sasa.

Hii ni baada ya Aisha kuvamia boma la Katana na kuzua rabsha.

Maribe alijibu,

"Wambui_glory tafadhali usinitaje kwa mambo usiyoyajua, asante," Maribe .