Jaguar alala jela usiku wa kuamkia leo, watu mashuhuri wamuunga mkono

Mbunge wa Starehe anayejulikana kwa jina lake la utani kama Jaguar alikamatwa siku ya Jumatano baada ya matamshi aliyotamka.

Jaguar anatarajiwa mahakamani hii leo ili kusomewa mashtaka ya kuchochea wapiga kura wake dhidi ya wageni.

Alilala usiku mzima katika seli za polisi za Kileleshwa.

Alipokuwa anatoa hotuba yake kwa wafanya biashara wa Kirinyaga, mwimbaji huyo alisema,

Ukitathmini masoko yetu yamechukuliwa na waganda na watanzania. Na ikiwepo hawatatolewa baada ya saa 24, tutawatoa kwa nguvu na kuwachapa na hatutaogopa yeyote.

Baada ya kutiwa mabaroni alijitetea akisema,

Matamshi niliyoyatamka jana yalikuwa yakiwalenga wachina ambao wamevamia soko na kufanya biashara za wanaanchi wa Kenya kuwa ngumu.

Maneno ya Jaguar hayaja wagawanya wabunge bali pia wakenya, wengine wame muunga mkono huku wengine wakimkemea.

Haya ni baadhi ya maoni yaliyotolewa

akotheekenya It shall be well

huddahthebosschick We shall Prevail!

terencecreative Pamoja milele

iamfrasha tuko na wewe 💯💯💯💯💯💯

allyabdu Mimi nisha rudi nipo kwetu Tanzania

djtibzkenya @jaguarkenya Nobody’s perfect, we all make mistakes, just apologize to our brothers and we all move on, we need each other now more than ever. Peace & love always.