Jamaa anayeshukiwa kuhusika na mauwaji ya mwanahabari Marjan atiwa mbaroni

Marjan-730x414
Marjan-730x414
NA NICKSON TOSI

Jamaa wa miaka 19 anahusishwa na mauwaji ya mwanahabari Mohammed Hussein Marijan ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi.

Mwanamke anayesemekana alipanga njama na kikundi cha watu sita pia anatafutwa na maafisa wa usalama.

“We still have a lot to do and we cannot disclose more details. We are, however, optimistic that all the people responsible for the killing will be brought to book,”Lucas Ogara OCPD wa  Kilimani amesema .

Marjan alikumbana na kifo chake eneo la Makina, mtaa wa Kibra mita chache tu kutoka kwa mahakama za Kibra akiwa anatoka kazini..

Taarifa zinasema kwamba mwanahabari huyo alikuwa mmoja wa wanakamati wa shirika la Kibera Policing Committe na aliuwawa kwa kudungwa kisu mara sita na kufa papo hapo.

Ogara aidha amesema wanaoendesha uchunguzi huo wataangazia sana kamera za siri ili kubaini waliotekeleza mauwaji hayo.