Jamaa apokea kichapo kwa madai ya kuhonga wapiga kura, Kibra

unnamed__1573109028_26977
unnamed__1573109028_26977
Hali tata imetokea katika eneo la Mashimoni Squatters baada ya jamaa kupata kichapo cha umma kwa kudaiwa kuwahonga wapiga kura.

Jamaa huyo kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa polisi huku uchunguzin ukiendelea kubaini madai hayo na huenda akafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Video inaonyesha maafisa wa polisi wakijaribu kuwazuia wananchi dhidi ya kumshambulia .

Kabla ya maafisa wa polisi kufika, jamaa huyo alikuwa tayari kapokea kichapo kutoka kwa wananchi waliokuwa na ghadhabu.

Haya yanajiri huku zoezi la kumtafuta mbunge wa Kibra likiendelea.

Mwanawe kinara wa upinzani Raila Odinga, Winnie Odinga tayari ashapiga kura na kuwahimiza wakaazi kujitokeza kupiga kura.

 Idadi ya wanaojitokeza katika vituo vya kupiga kura inaonekana kuwa ndogo mno.

Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa mapema saa kumi na mbili asubuhi katika wodi zote 5 za Kibra.

Vituo hivi ni Sarang'ombe, Woodley ,Golf Course, Laini Saba na Lindi.

Katika baadhi ya vituo,mashine za kidigitali zilifeli huku zingine zikikosa kuwaka.