Jamaa Migori akojolea kitanda baada ya kunyimwa tendo la ndoa

Kama wewe ni shabiki sugu wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, basi unajua bayana kwamaba kila siku ya wiki kabla ya kitengo cha Patanisho, kuna kitengo cha Story za Ghost.

Katika kitengo hiki, bwana Ghost Mulee huwa na fursa ya kuwapa waskizaji wa Radio Jambo pamoja na Gidi, uhondo wa kufurahisha uliotokea kote duniani.

Basi siku ya Jumanne, bwana Ghost alisimulia kisa kilichotokea Migori ambapo inakisiwa jamaa fulani aliyejawa na hamaki aliamua kukojolea kitanda chake. Kisa na maana? Alinyimwa tendo la ndoa na mkewe.

Kulingana na Ghost, jamaa huyu alienda kubugia pombe na kurudi usiku wa maneno akiwa mlevi kupindukia.

Jamaa aliporudi alimuamsha mkewe akimuomba tendo la ndoa, mkewe ambaye alikuwa ameshinda kazini siku mzima alikuwa amechoka na hangekubali.

Yule jamaa alikasirika sana na ili kulipiza kisasi, alikojolea kitanda chao jambo lililomkasirisha mkewe na kuondoka na watoto wao watatu.