Jamaa wa miaka 52 akamatwa kwa makosa ya kukuza bangi

Baba wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 52, kutoka kijiji cha Mugumo kata ndogo ya Githunguri, Ol Kalou jana jioni alijipata taabani baada ya kukamatwa kwa makosa ya kukuza bangi.

John Mwangi alikuwa amepanda mimea ya bangi katika ua (fence) lake na mimea kadhaa ndani ya nyumba yake.

Wakazi wa eneo hilo waligundua 'mmea' huo baada ya kufungua paa lake ili aupatie nafasi ya kutosha urefuke na wakamjulisha mzee wa kijiji ambaye baada ya kumjulisha naibu wa chifu wa eneo la Githunguri, bwana Pascal Gathima.

Pascal naye aliwajulisha wakubwa wake na hapo afisa wa polisi wakapanga kumkamata.

Jana jioni, OCS wa Ol Kalou Moses Munyoki aliongoza kikosi ambacho kilikuwa na maafisa wa polisi hadi nyumbani kwake Mwangi ambako alikamatwa na mumea huo kung'olewa.

Mwangi akijitetea alisema kuwa rafikiye kutoka Kirinyaga alimpa mbegu ambazo alipanda wakielewana kuwa atamrudishia baada ya kuvuna na katika ile harakati angejipatia elfu 20,000. Anasema kuwa alipanda mwezi wa Aprili.

Naibu wa chifu Pascal Gathima alisema hawana mengi ya kusema kumhusu mshukiwa huyo kwani pia hajakuwa nyumbani kwake kwa mda mrefu na hakuna aliyeshuku kuwa anakuza bangi kwake.