Jamii yadai haki baada ya wana wao kuuwawa na umati kule Saboti

65479204_117399972851849_734547579659053846_n
65479204_117399972851849_734547579659053846_n
Familia ya mwanafunzi aliyeuawa wa chuo kikuu cha Masai Mara wameapa kwamba hawatamzika mtoto wao iwapo haki itatokea.

Collins Kibet aliyejulikana kama Oliver, alikuwa mwanafunzi wa biashara na Dan Kipsang mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Holy Trinity ilio jimbo la Saboti.

Wawili hao walishambuliwa na kuuawa na umati wa watu wiki iliyopita.

Kulingana na chanzo cha habari hizo, Oliver alikuwa ameandamana Dani saa 11 usiku hadi eneo jirani la Kinyoro ambapo alikuwa ameenda kumwona msichana.

Saa 11 usiku mama wa wasichana hao aligundua kuwa kulikuwa na wavulana katika chumba cha wasichana na hapo aliufunga mlango kutoka nje na kupiga kelele akidai kuwa kulikuwa na wezi.

Chanzo cha habari hiyo ziliendelea na kusema kuwa majirani walikuja na kuwashambulia wawili hao na kuwapiga hadi kufa. Lakini swali lilioibuka ni kwanini maafisa wa KPR walitembelea katika eneo hilo na kuondoka bila kuokoa hali hiyo.

"Sitamzika mwanangu kama haki haitakuwapo, mwanangu aliuawa kikatili bila kosa, ninajitahidi kumfundisha kwani alikuwa mwenyekwa bidii lakini usalama ulishindwa kumlinda," mama ya Evelyn Temko Oliver alisema akidodokwa na machozi.

Temko alikuwa akizungumza nyumbani kwake, kijiji cha Sukwo eneo la Saboti ambapo wana Mca na waweka usalama wakiongozwa na Kamishna wa Kaunti ya Trans Nzoia Sam Ojwang walikuwa wametembelea kutoa pole zao.

Bwana Ojwang alithibitisha kuwa watuhumiwa wawili wamekamatwa wakati wengine watano bado wanafuatwa.

"Tunataka kuhakikishia familia zilizoathiriwa kuwa hatutapumzika hadi watuhumiwa wote watakapokamatwa, tunawasihi pia jamaa za watuhumiwa waliokosekana watupe habari za waliopo," alisema.

"Uhalifu umetekelezwa na watu binafsi na sio jamii kwani mizozo hio inaweza kusababisha ukabila hasi," alisema.

Aliwataka jamii kuwa na subira na iwape muda wa kukamilisha uchunguzi wao.

Som mengi