Avamia mtoto wa shule akioga bafuni, kisa chasimuliwa

andrew
andrew
Jamaa mmoja amefikishwa kortini na kushtakiwa kwa tuhuma za kumbaka msichana wa umri wa miaka 15.

Msichana huyu alikuwa akioga katika bafu mtaani Kangemi viunga vya jiji la Nairobi.

Andrew Mackezie mwenye umri wa miaka 37, anatuhumiwa kwa kuvamia mlango wa bafu ambayo msichana huyo alikuwa akioga.

Mwendesha mashtaka alielezea korti hiyo kuwa Mackenzie alimwacha mkewe ndani ya nyumba na kuondoka nje haraka baada ya kumuona msichana huyo akielekea bafuni.

Inadaiwa Mackenzie alitumia kitambaa kufunika mdomo wa msichana huyo ili asipige nduru.
Aidha alimtishia kuwa atamuua iwapo ataelezea mtu yeyote kuhusu kisa hicho.

Afisa huyo alisema kuwa msichana huyo aliendelea kuoga baada ya tukio hilo na kuenda shuleni bila kusema neno lolote.

Ripoti za polisi zinaonyesha kuwa mwalimu wa msichana huyo aligundua kuwa msichana huyo alikuwa na wasiwasi.

Wakati wa mapumziko, msichana huyo alienda akaripoti kisa hicho kwa katibu wa shule hilo.

Mwalimu mkuu alimpigia mamake msichana huyo aje shuleni na baadaye walienda hospitalini kabla ya jambo hilo kuripotiwa kwa polisi.

Mtuhumiwa alikamatwa baadaye na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kabete, kisha baadaye alipelekwa kortini na kushtakiwa.

 Mackezie alikana mashtaka hayo wakati alipofikishwa mbele ya hakimu wa Kibera Barbara Ojoo.

Hakimu huyo alimpa dhamana ya shilingi 300,000 na dhamana ya kiasi kama hicho.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba tarehe nane, kabla ya kusikilizwa mwezi wa Novemba tarehe kumi na moja.